1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu Wanajeshi wa Ethiopia washambuliwa .

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHT

Taarifa kutoka mji mkuu wa Somalia-Mogadishu, zinasema watu wenye wamepambana na majeshi ya Ethiopia na serikali ya mpito wakitumia makombora baada ya kuishambulia bandari ya mji huo na makao makuu ya idara ya zamani ya usalama. Watu wawili waliuwawa na wengine wanne kujeruhiwa. Hujuma hizo za waasi zinasemekana zililengwa dhidi ya maeneo manne tafauti Mashambulio hayo yametokea wakati ujumbe wa watu 18 wa umoja wa mataifa ukiongozwa na Naibu katibu mkuu anayehusika na masuala ya kisiasa Tuliameni Kalomoh, ukiwasili Baidoa , kilomita 250 kusini magharibi mwa Mogadishu, na mahala lilipo bunge la mpito la Somalia.