1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wanajeshi wa kulinda amani wawasili

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLs

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika kutoka Uganda kimewasili leo mjini Mogadishu nchini Somalia kuanza kibarua chao kigumu cha kulinda amani nchini humo.

Wanajeshi hao ni sehemu ya jeshi la Umoja wa Afrika litakalokuwa na wanajeshi 8,000 lenye lengo la kuilinda serikali dhaifu ya mpito ya Somalia na kuwapa nafasi wanajeshi wa Ethiopia waondoke Somalia.

Ndege nne za kubeba mizigo zilizowabeba wanajeshi hao zilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu chini ya ulinzi mkali.

Wanajeshi hao wamelakiwa na maafisa wa serikali ya mpito ya Somalia na wababe wa kivita wanaoudhibiti mji mkuu Mogadishu.