1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wanajeshi wa Somalia washambuliwa

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcM

Watu waliokuwa wamejihami na bunduki waliwashambulia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia mjini Mogadishu hapo jana.

Wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia inayoongozwa na waziri mkuu, Ali Mohamed Gedi, walifaulu kuwatimua wanamgambo wa mahakama za kiislamu kutoka mjini Mogadishu wiki iliyopita.

Mjumbe maalumu wa Marekani barani Afrika, Jendayi Frazer, amesema ipo haja ya kupeka kikosi nchini Somalia kuzuia kurejea enzi ya wababe wa kivita.

´Ni wazi kwamba tunahitaji mtu mwingine aingie Somalia. Wasomali hawana jeshi la taifa wala polisi. Tuna jukumu la kuzuia kurudi kwa enzi ya wababe wa kivita. Kwa hiyo tunahitaji kupeleka kikosi ambacho hakitapendelea upande wowote nchini Somalia.´

Mamia ya wasomali waliokuwa na hasira walifanya maandamano juzi Jumamosi ya kupinga nchi yao kukaliwa na majeshi ya Ethiopia na mpango wa serikali wa kuwapokonya silaha.