1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wanajeshi zaidi wa Ethiopia waingia Somalia

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC6

Wanajeshi zaidi wa Ethiopia wameingia nchini Somalia siku tano baada ya kusimamishwa mapigano yaliyoukumba mji mkuu wa Mogadishu.

Wakaazi wa mji wa Baidoa ulio kilomita 250 kaskazini magharibi mwa Mogadishu wamesema kuwa ndege mbili za kijeshi za Ethiopia zilitua tangu jana na wanajeshi hao wameelekea mjini Mogadishu.

Ethiopia hata hivyo imekanusha kuwapeleka wanajeshi wake zaidi nchini Somalia.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umeonya kuwa huwenda Ethiopia,Somalia na kikosi cha kulinda amani cha umoja wa nchi za Afrika zilitenda uhalifu wa kivita katika siku nne za machafuko yaliyokumba mji wa Mogadishu.