1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wanamgambo wa Somalia wajaribu makombora

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwM

Ripoti zinasema,wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia wamefanya majaribio ya makombora na wanajitayarisha kuvishambulia vikosi vya serikali ya mpito.Wanamgambo hao wanadai kuwa vikosi hivyo vinasaidiwa na majeshi ya Ethiopia.Kuna hofu ya kuzuka vita,baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani,kati ya wanamgambo wanaodhibiti Mogadishu na sehemu kubwa kusini mwa nchi na serikali ya mpito,inayoungwa mkono na nchi za magharibi.