1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Wasomali wafikia makubaliano.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HF

Waziri mkuu wa Somalia Ali Mohammed Gedi amefikia makubaliano ya amani na ukoo maarufu wa hawiye ambao baadhi ya wapiganaji wake walikuwa wakiwaunga mkono wanamgambo wa mahakama za Kiislamu katika vita vyao dhidi ya majeshi ya serikali ya mpito na vikosi vya Ethiopia mapema mwaka huu.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya wazee wa ukoo huo wa Hawiye kukutana na waziri Ali Mohammed Gedi mjini Mogadishu. Akizungumza baada ya mazungumzo hayo waziri mkuu Gedi alisema, viongozi wa ukoo huo wawekubali kushirikiana na serikali katika kupambana dhidi ya wapiganaji.

Wakati huo huo kiongozi muhimu wa Somalia ametoa wito wa kupigana vita takatifu Jihad leo, akiapa kuwa mapigano dhidi ya serikali inayoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia mjini Mogadishu yatamalizika iwapo sheria za Kiislamu zitarejeshwa.