1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:10 wauawa katika ghasia za mjini

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYr

Watu wanane wameuawa mjini Mogadishu kufuatia mapigano kati ya majeshi ya Ethiopia yanayounga mkono jeshi la serikali ya muda ya Somalia na wanamgambo.Majehsi hayo yanatia juhudi kudumisha amani mjini humo.Wanajeshi 5 walipoteza maisha yao pale gari walimokuwamo kulipuka kwenye bomu la kutegwa ardhini mkoani Arafat ulio kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.Eneo hilo linaaminika kuwa la ghasia nyingi.

Raia mmoja aliuawa kusini mwa Mogadishu kwenye mkoa wa Blacksea wakati wanamgambo waliporushia kikosi cha jeshi walioshika doria guruneti.Tukio hilo lilisababisha wanajeshi hao kulipiza kisasi.Haijulikani iwapo kifo cha mtu huyo kilisababishwa na mlipuko au risasi.Watu wengine wawili wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko wa guruneti kwenye soko mjini Afgoye ulio takriban kilomita 30 magharibi mwa Mogadishu.Wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Ghasia hizo zimesababisha vifo vya watu 30 katika kipindi cha siku mbili zilizopita.Somalia inazongwa na ghasia tangu utawala wa Rais Mohamed Siad Barre kungolewa mwaka 91.

Mkutano wa maridhiano ya kimataifa unaendelea mjini Mogadishu ila kususiwa na mahakama za kiislamu vileviole wawakilishi wa ukoo mkubwa wa Hawiye.