1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Ghasia zaidi Mogadishu zasababisha maafa

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGr

Takriban watu 14 wamepoteza maisha yao wakiwemo wanajeshi 6 wakati mapigano makali yakiendelea kusini mwa mji wa Mogadishu.Hii inatokea baada ya kambi ya kijeshi ya majeshi ya Ethiopia kushambuliwa kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Wakati huohuo Majeshi ya serikali ya muda ya Somalia yakishirikiana na ya nchi jirani ya Ethiopia yalishambulia ngome moja ya wanamgambo mjini Mogadishu .Wapiganaji hao walililipiza kisasi kwa kurusha makombora wakiwa wamejificha katika ngome yao.

Kwa upande mwingine viongozi wa serikali ya Somalia wanapanga kuwashambulia wanamgambo hao ili kuwamaliza nguvu.Hata hivyo Rais wa Somalia Abdillahi Yusuf anashukuru majeshi ya Uganda walioko nchini humo kulinda amani.

Majeshi ya Uganda yaliwasili nchini Somalia mwezi huu katika mpango wa Umoja wa Afrika wa kupeleka majeshi alfu 8 ya kulinda amani Somalia baada ya Serikali ya muda kuwafurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu kwezi Disemba mwaka jana.