1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Hali ya utulivu yarejea Mogadishu huku wanajeshi wakipiga doria

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC68

Wanajeshi wa Somalia na Ethiopia pamoja na maafisa wa polisi wanaendelea kupiga doria kwenye mji mkuu Mogadishu baada ya kupatikana utulivu wa kiasi.

Maafisa hao wanafanya msako wa magari kutafuta silaha ambazo huenda zimefichwa.

Hii inakuja baada ya zaidi ya wiki moja ya mapigano makali kwenye mji huo.

Wakaazi wa Mogadishu wameiondoa miili ya watu waliouwawa kwenye vita na kuandaa mazishi hii leo.

Serikali ya mpito ilidai ushindi hapo alhamisi na ikisema ni wapiganaji wacahache tu waliosalia katika mji huo na watafanya juhudi za kuwamaliza hivi karibuni.

Makundi ya haki za binadamu mjini humo yamesema mapigano yalisababisha kuuwawa kwa watu zaidi ya 1000 na wengine laki nne wamekimbia makaazi yao.