1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Majeshi ya serikali yashambulia wapiganaji

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EZ

Majeshi ya Serikali ya muda ya Somalia yamepambana na wapiganaji wa mahakam za kiislamu kwenye eneo la kusini mwa Mogadishu na kusababisha vifo vya watu wawili.Pande zinazohasimiana zilipambana kwa kutumia silaha nzito nzito jambo lililosababisha wakazi wa eneo hilo kubaki majumbani mwao huku wengine wakitoroka kwa kuhofia usalama wao.

Wapigananaji wa mahakama za kiislamu waliofurushwa mjini Mogadishu na majeshi ya serikali ya Somalia yakishirikiana na majeshi ya nchi jirani ya Ethiopia bado wanashambulia mji huo.

Somalia imezongwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 91 baada ya Mohamed Siad Barre kungolewa madarakani.Juhudi za kutafuta amani nchini humo zimeambulia patupu.