1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Makombora yashambulia ukumbi wa mkutano wa amani

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiC

Makombora 7 yamelipuka mjini Mogadishu wakati mkutano wa amani nchini Somalia ulipofunguliwa hapo jana.Tukio hilo lilisababisha kikao hicho kuahirishwa ili kuwapa wajumbe muda zaidi wa kuwasili.Rais Abdillahi Yusuf wa Somalia alikuwa akihutubia kikao hicho wakati milipuko ilipotokea jambo aliendelea na ratiba yake.

Kulingana na afisa wa polisi Ibrahim Dhagool makombora mawili yaliripuka mkoani Shibis karibu na ukumbi wa mkutano .Hakuna majeruhi wowote walioripotiwa.Makombora mengine matano yalishambulia eneo la makazi na kujeruhi watu 3.

Baada ya muda mfupi mwandalizi wa mkutano huo Ali Mahdi Mohammed aliahirisha kikao hadi siku ya Alhamisi ili kuhakikisha kuwa wajumbe wote wanahudhuria.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali wajumbe ya wajumbe 1325 wamealikwa kuhudhuria mkutano huo.

Maafisa wakuu waliohudhuria mkutano huo ni Spika wa Bunge Aden Mohamed Nur,waziri wa Ethiopia Tkeda Alamu na Atalla al Bashir kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya eneo la Pembe ya Afrika ,IGAD.Mkutano huo umeshaahirishwa mara tatu kwasababu ya ukosefu wa fedha.Kikao hicho kinalenga kujadilia namna ya kugawana madaraka kati ya koo nne kubwa na moja ndogo.