1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mapigano mapya yazuka 12 wauawa

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKa

Mapigano makali yametokea kati ya majeshi ya majeshi ya Somalia yanayoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia na wapiganaji wa mahakama za kiislamu.Pande zote mbili zinadai kusababisha majeruhi wengi.Mapigano hayo ya usiku kucha yalitokea katika makao ya zamani ya Wizara ya Ulinzi kuisini mwa Mji wa Mogadishu na kusababisha moto katika soko la Bakar ambako wanamgambo hao wa kiislamu huvamia polisi wanaoshika doria.

Sheikh Mukhtar Robo Abu Mansur ambaye ni kamanda wa vuguvugu la Shabab mjini Mogadishu anasema kuwa wapiganaji wake waliwaua wanajeshi 12 wa Somalia na 5 wa Ethiopia.Aliyasema hayo alipozungumza na shirika la habari la AFP.Sheikh Robo ni mwanachama wa ngazi za juu katika vuvugu la mahakama za kiislamu lililofurushwa mwezi Januari na jeshi la Somalia likishirikiana na jeshi la Ethiopia.Kulingana na kiongozi huyo majeshi ya serikali yanashambulia soko la Bakara kwa makusudi ili kuharibu mali ya raia.

Msemaji wa polisi Abduwahid Mohamed anakanusha madai hayo na kuongeza kuwa majeshi ya serikali yamewaua wanamgambo 13 na kupoteza mwanajeshi mmoja pekee.

Vuguvugu la Shabab ni wapiganaji walio na msimamo mkali wa Mahakama za Kiislamu waliomiliki sehemu kubwa ya eneo la kuisni na kati la Somalia mwaka jana.