1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU.Marekani yataka kurudi tena nchini somalia

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoX

Baada ya kushindwa vibaya mara mbili nchini Somalia Marekani sasa inajaribu tena kuingilia kati maswala ya nchi hiyo ya upembe wa Afrika hatua ambayo imeonywa na baadhi ya duru za kidiplomasia za barani Ulaya na katika bara la Afrika.

Wanadiplomasia hao wanaonya kuwa hatua ya Marekani itasababisha machafuko katika eneo hilo la upembe wa Afrika baina ya serikali ya mptio ya Somalia inayo ungwa mkono na Ethiopia na Utawala wa Kiislamu wenye nguvu unaoungwa mkono na Eritrea.