1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mlipuaji wa kujitolea muhanga auawa

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBus

Majeshi ya Ethiopia yamempiga risasi hadi kufa mlipuaji mmoja wa kujitolea muhanga na kulipua gari lake lilipokuwa likielekea katika makao yao makuu mjini Mogadishu.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama aliyezungumza na shirika la habari la Reuters mwanajeshi mmoja wa Ethiopia aliyekuwa kwenye paa la nyumba alimpiga risasi mlipuaji huyo jambo lililosababisha gari lake kuripuka