1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU.Wanamgambo watishia kuwauwa wafanyikazi wawili wa CARE

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2P

Wanamgambo waliowateka nyara wafanyikazi wawili wakigeni wa mashirika ya kutoa misaada kaskazini mwa Somalia wiki iliyopita,wametishia kuwauwa ikiwa utawala wa eneo hilo utajaribu kuanzisha opresheni ya kuwakomboa.

Abdiqani Hassan mwandishi wa habari wa shirika la Reuters alizungumza na kiongozi wa kundi hilo la watekaji nyara kwa njia ya mawasiliano ya simu na kiongozi huyo aliyejitaja kwa jina moja la Mohamed alisema mazungumzo ya wazee wa kimbari juu ya kuwaachilia huru wafanyikazi hao yamevunjika.

Wafanyikazi hao wa shirika la kimataifa la kutoa misaada la CARE ni raia wa Kenya na Uingereza.

Hata hivyo maafisa wa jimbo la Puntland na shirika hilo la CARE hawakupatikana kuzungumzia suala hili.