1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watoto wawili washambuliwa kwa bomu

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVs

Mlipuko wa bomu kandokando ya barabara mjini Mogadishu umesababisha vifo vya watoto wawili waliokuwa wakielekea shuleni hii leo.Watoto hao walikuwa wanatembea katika mtaa wa Gupta ulio kaskazini mwa mji huo kabla ya mlipuko huo kuwakata vipande vipande na kumjeruhi mzee mmoja.

Bado haijulikani aliyelengwa na bomu hilo lilitokea siku moja baada ya wapiganaji wa kiislamu kusisitiza kuwa wanaendelea na mashambulizi mpaka wanajeshi wa Ethiopia wanaounga mkono jeshi la serikali ya Somalia waondoke nchini humo.

Serikali ya Somalia inafanya mkutano wa kutafuta amani na maridhiano ya kitaifa japo kikao kinasusiwa na wapiganaji wa kiislamu aidha jamii ya ukoo wa Hawiye ulio na ushawishi mkubwa nchini humo.Kikao hicho kinafadhiliwa na Umoja wa mataifa na mataifa ya magharibi.Somalia inakabiliwa na ghasia tangu kuongolewa madarakani kwa Siad Barre mwaka 91.