1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watu 11 wauawa, baada ya kikosi cha AU kushambuliwa

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLE

Watu 11 wameuawa mjini Mogadishu huko Somalia baada ya wanamgambo wa kisomali kukishambulia kikosi cha kulinda amani cha umoja wa afrika.

Kwa mujibu wa mashuhuda, maroketi yaliyolengwa kwa jeshi hilo la umoja wa afrika, yalianguka katika mgahawa mmoja mjini Mogadishu na kuwaua watu tisa.

Mapema watu wawili waliuawa katika mapambano kati ya wanamgambo hao wa kisomali na jeshi hilo la umoja wa afrika.

Majeshi ya muungano wa mahakama za kiislam yalifurushwa na majeshi ya Ethiopea yaliyokuwa yakiisadia serikali ya mpito ya Somalia mwezi desemba mwaka jana.

Hata hivyo wanamgambo hao wa kiislam waliapa kuwa watayashambulia majeshi yoyote ya kigeni yakayoingia Somalia.

Kikosi cha kwanza cha Umoja wa Afrika, ambacho ni jeshi la Uganda kiliwasili nchini Somalia wiki hii kuchukua nafasi ya majeshi ya Ethiopea.Umoja wa Afrika umepanga kupeleka jeshi la askari elfu 8.