1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watu 7 wauawa katika mapigano mapya

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWU

Majeshi ya usalama ya serikali ya muda ya Somalia wamewaua wanamgambo 7 na mmoja wao kupoteza maisha yake katika mapigano makali mjini Mogadishu.Kwa mujibu wa msemaji wa polisi mwanajeshi mmoja wa serikali aliuawa pale wanamgambo waliposhambulia kituo kimoja cha polisi kwenye eneo la kaskazini la SOS huku ghasia katika kambi moja ya kijeshi ya zamani iliyo katika mkoa wa kusini wa Shirkole kusababisha vifo vya wanamgambo 7.

Mapema mwaka huu Majeshi ya Ethiopia yanayoshirikiana na jeshi la Somalia yaliwafurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu waliodhibiti maeneo kadhaa ya nchi.Tangu wakati huo wanamgambo wa kiislamu wanashambulia serikali katika mji mkuu wa Mogadishu kila siku.Mazungumzo ya kutafuta maridhiano ya kitaifa hayajafua dafu kwani wapiganaji wa kiislamu wanasusia vikao hivyo aidha idadi kubwa ya ukoo mkubwa wa Hawiye ulio na ushawishi mkubwa nchini humo.