1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU.:Watu 70 wauawa mjini Mogadishu

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKG

Watu zaidi ya 70 wameuawa mjini Mogadishu kutokana na mapigano makali baina ya wapinzani na majeshi ya serikali ya Somalia yanayosaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia.

Duru za hospitali zimesema watu wenginezaidi ya mia mbili walijeruhiwa katika mapigano hayo yaliyochukua muda wa siku mbili.

Habari zaidi zinasema majeshi ya Ethiopia yanafanya mashambulio ya kulipiza kisasi baada ya askari wao kuuawa na miili yao kuvurutwa mitaani.

Maalfu ya watu wameukimbia mji wa Mogadishu kutokana na mapambano ya kupigania udhibiti wa mji huo baina ya wapinzani wa mabaraza ya kiislamu na majeshi ya serikali ya Somalia yanayosaidiana na ya Ethiopia.