1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU.watu saba zaidi wauwawa

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVo

Takriban watu saba wameuwawa katika mashambulio ya makombora katika mji mkuu wa Mogadishu.

Watu kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio jingine la kombora lililolenga kusini mwa mji wa Mogadishu katika kijiji cha Barakat .

Hali hiyo inaashiria hali ya ukosefu wa usalama nchini Somalia huku umoja wa nchi za Afrika ukipanga kuwapeleka wanajeshi wake 8000 wa kulinda amani.

Zoezi hilo hadi sasa lakini limekusanya nusu tu ya idadi ya wanajeshi wanaohitajika.