1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA : Shehena ya silaha yagunduliwa

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbb

Serikali ya Liberia inayochunguza uwezekano wa njama ya mapinduzi imegunduwa shehena kubwa ya silaha mpya za bunduki aina ya AK -47 katika mji mmoja ulioko kwenye barabara inayoelekea Ivory Coast.

Msemaji wa polisi Alvin Jask Kanneh amesema ni mapema mno kusema iwapo shehena hiyo ya silaha zilizofichwa ina uhusiano na mpango unaodaiwa wa usafirishaji wa magendo ya silaha nchini Liberia kutoka Ivory Coast.

Mkuu wa zamani wa majeshi na spika wa zamani wa bunge wamefunguliwa mashtaka ya uhaini mwezi uliopita kuhusiana na njama hiyo.