1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Washukiwa njama ya mapinduzi wakamatwa Liberia

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhQ

Aliekeuwa mkuu wa majeshi nchini Liberia amekamatwa kwa kushikiwa kula njama ya kutaka kuipindua serikali.Naibu waziri wa habari wa Liberia,Gabriel Williams amesema,Charles Julu aliekuwa mkuu wa majeshi katika serikali ya rais wa zamani Samuel Doe,amekamatwa pamoja na watu wengine watano.Akaongezea kuwa habari zaidi zitatolewa baadae,kwani hivi sasa Julu na wenzake wanafanyiwa uchunguzi.