1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Kituo cha Bo Waterside chafunguliwa baada ya miaka 17

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtk

Liberia na Sierra Leone zimefungua eneo lao la mpakani baada ya miaka 17.Eneo hilo Bo Waterside linalotumika kwa biashara lilifungwa mwaka 90 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuchipuka kati ya chama cha Rais wa Liberia wa zamani Charles Taylor National Patriotic Party of Liberia, NPFL kupambana na uongozi wa kiongozi wa wakati huo Samuel Doe.

Kufunguliwa kwa kituo hicho cha Bo Waterside cha mpakani kunatarajiwa kuimarisha biashara kati mataifa hayo mawili jirani yanayojijenga upya baada ya kipindi kirefu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe.