1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONTEBELLO:Bush katika mkutanao na wakuu wa Canada na Mexico

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBX9

Rais George Bush wa Marekani pamoja na viongozi wa Canada na Mexico wanatarajiwa kuzidisha ushirikiano zaidi katika kile kinachoziunganisha nchi hizo na kuainisha kasoro zilizoko.

Rais Bush anajaribu kuimarisha uhusiano na nchi hizo katika mkutano wake na Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper pamoja na Rais Felipe Calderon wa Mexico, huko katika mji wa Montebello pembezoni mwa mto Ottawa Canada.

Wanatarajiwa angalau kufikia makubaliano katika baadhi ya maeneo ikiwa ni juhudi za kuainisha mipango ya ulinzi wa mipakani.