1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Montevideo. Bush ataka mazungumzo ya WTO yafufuliwe.

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKL

Rais wa Marekani George W. Bush ambaye yuko nchini Uruguay katika sehemu ya pili ya ziara yake ya mataifa matano ya Latin Amerika , ametoa wito wa kufufuliwa kwa mazungumzo ya shirika la biashara la dunia. Alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Uruguay, Tebare Vazquez, baada ya mkutano baina ya viongozi hao wawili.

Ulinzi ulikuwa mkubwa katika mji mkuu Montevideo kufuatia ghasia za maandamano kabla ya ziara ya kiongozi huyo wa Marekani.

Bush aliwasili akitokea Sao Paulo, Brazil , ambako maelfu ya waandamanaji pia waliingia mitaani.

Mkutano wa rais Bush na rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ulilenga katika kuendeleza mafuta ya Ethanol kama nishati mbadala.

Wakati huo huo , rais wa Venezuela Hugo Chavez , ambaye anafanya ziara nchini Argentina , alimshambulia Bush, akimwita maiti ya kisiasa wakati wa mkutano mkubwa mjini Buenos Aires.