1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morgan Tsvangirai apata ajali ya gari

P.Martin - AFPE7 Machi 2009

Waziri Mkuu mpya wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea siku ya Ijumaa kusini ya mji mkuu Harare.

https://p.dw.com/p/H7I3
Morgan Tsvangirai, leader of the main opposition party in Zimbabwe at a press conference in Harare, Wednesday, June, 25, 2008. Tsvangirai called on African leaders to assist in negotiating a solution in Zimbabwe as he spoke to reporters Wednesday about his country's political crisis. He repeated his rejection of a presidential runoff set for Friday. (AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC.Picha: AP

Msemaji wa chama cha Morgan Tsvangirai cha MDC,James Maridadi amesema,Susan Tsvangirai,mke wa waziri mkuu aliekuwemo katika gari hilo amefariki dunia.Ajali hiyo ilitokea walipokuwa njiani kwenda nyumbani kwao wilayani Buhera.Ripoti zinasema,gari hilo lilipinduka mara tatu baada ya kugongwa na lori.

Morgan Tsvangirai,kiongozi wa chama cha MDC,aliapishwa waziri mkuu wa Zimbabwe tarehe 11 mwezi wa Februari kufuatia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na Rais Robert Mugabe wa ZANU-PF.Wengi wana matumaini kuwa Morgan Tsvangirai mwenye miaka 56 atasaidia kuimarisha uchumi wa Zimbabwe ulioporomoka vibaya.Wengine wana wasiwasi kuwa anagawana madaraka na Robert Mugabe.

Takriban nusu ya wananchi wanategemea msaada wa chakula kutoka nje na hali hapo zamani Zimbabwe ilikuwa ikilisha nchi zingine barani Afrika.Hata mifumo ya miundombinu na huduma za afya zinahitaji kufanyiwa ukarabati wa dharura. Ugonjwa wa kipindupindu ulioripuka nchini humo tangu mwezi wa Agosti mwaka 2008 umeua watu 4000 na wengine 80,000 wameambukizwa ugonjwa huo.