1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MORONI:Kanali Mohamed Bakary aunda serikali ya kujipa uhuru

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaX

Rais wa Nzouani visiwani Komoro ameunda serikali ya kujiweka huru.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali hiyo mpya Arbabidine Mohamed lengo lao ni kukiweka kisiwa hicho huru kwa njia yoyote ile.

Kisiwa cha Nzouani ni sehemu ya serikali kuu ya Komoro inayojumuisha visiwa vya Ngazija na Moheli.Kisiwa cha Nzouani kimekuwa na matatizo na serikali kuu ya Komoro baada ya Kanali Mohamed Bakary kulazimisha uchaguzi na kuapishwa kinyume na agizo la Umoja wa Afrika.,

Umoja wa Afrika unamlaumu Kanali Mohamed Bakary kwa kuingilia juhudi za kuimarisha uhusiano katika visiwa vya Komoro.

Visiwa vya Komoro vimezongwa na mivutano kati ya maeneo matatu husika Moheli,Ngazija na Nzouani huku serikali kuu ikikabiliwa na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 75.