1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Belarus kukosa gesi mwakani?

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfe

Kampuni kubwa la uuzaji wa Gesi nchini Russia Gazprom limetishia kusitisha kuipatia huduma hiyo Belarus ifikapo Januari mosi hadi pale nchi hiyo itakapokubaliana na ongezeko kubwa la bei ya bidhaa hiyo.

Mkuu wa kampuni la Gazprom Alexei Miller amesema katika mahojiano ya televisheni kuwa kampuni lake imezionya nchi za mataifa ya magharibi kuwa usambazaji unaweza kuathirika. Gazprom linadai kuwa Belarus ilipe zaidi ya mara mbili ya bei ya sasa kwa ajili ya gesi mwakani na kutoa kiasi cha asilimia 50 ya hisa za mfumo wa usambazaji wa gesi nchini humo.

Hii ni mmoja kati ya mizozo kadha kati ya Russia na majirani zake juu ya bei wanayolipa kwa ajili ya gesi.