1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Georgia kupandishiwa bei ya gesi maradufu

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwa

Urusi imesema inapanga kuongeza maradufu bei yake ya gesi inayouzwa kwa Georgia baada ya mazungumzo kati ya nchi hizo mbili kushindwa kutatuwa mvutano wao na kukomesha hatua ya Urusi ya kuizulia gesi nchi hiyo.

Ofisa wa kampuni inayohodhi biashara ya gesi nchini Urusi ya Gazprom amesema kampuni hiyo imependekeza kupandisha bei ya kawaida ya gesi ya mchemraba 1,000 kutoka dola 110 hadi kuwa dola 230.Pendekezo hilo limekuja wakati mazungumzo ya ngazi ya juu yakiwa yameshindwa kutatuwa mzozo mkali ulioanza pale Georgia ilipowakamata maafisa wanne wa kijeshi wa Urusi hapo mwezi wa Septemba na kuwatuhumu kwa ujasusi.

Juu ya kwamba maafisa hao baadae waliachiliwa huru Urusi iliweka vikwazo kadhaa dhidi ya Georgia.