1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Iran yaitaka Urusi ikamilishe ujenzi wa kinu cha Bushehr

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQb

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran, Manoucher Mottaki, leo anatarajiwa kuishinikiza Urusi ikamilishe ujenzi wa kinu cha nyuklia cha Bushehr, katika mazungumzo ambayo huenda yakagubikwa na wasiwasi wa Urusi kuhusina na mpango wa nyuklia wa Iran.

Akiwa ziarani mjini Moscow, waziri Mottaki amepangiwa kukutana na kiongozi wa shirika la nyuklia la Urusi, Sergei Kiriyenko, ambalo matawi yake yanajenga kinu cha nyuklia cha Bushehr nchini Iran.

Wahandishi wa Urusi wameahirisha kukamilisha ujenzi wa kinu hicho katika ghuba ya Persia hivyo kuzusha hali ya wasiwasi kati ya serikali ya Moscow na Iran.

Urusi inasema inakabiliwa na matatizo ya kifedha kukamilisha ujenzi wa kinu cha Bushehr, lakini wadadisi wanasema haimuamini rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad na inahofia hatua za jumuiya ya kimataifa iwapo itaipelekea Iran nishati ya nyuklia katika kinu cha Bushehr.