1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Marekani itaendelea na mradi wa makombora ya kujikinga

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrc

Urusi imetoa mwito kwa Marekani kusitisha kwa hivi sasa mpango wake wa kutaka kujenga vituo vya makombora ya kujikinga nchini Poland na Jamhuri ya Czech.Hapo awali waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates alisema,Washington itaendelea na mpango wake wa kujenga vituo vya kinga katika Ulaya ya Mashariki licha ya mradi huo kukosolewa na Urusi.Waziri Gates alitamka hayo kwenye mkutano wa Shirika la Kujihami la Magharibi-NATO na Urusi mjini Brussels.Vile vile alimuambia waziri mwenzake wa Urussi,Anatoly Serdyukov, pendekezo lililotolewa na Moscow la kuwa na mradi wa pamoja wa rada nchini Azerbaijan,utakuwa ziada ya ule mpango wa Marekani nchini Poland na Jamhuri ya Czech.Serikali ya Moscow inaupinga mpango huo wa Marekani na hutazamwa kama ni kitisho kwa usalama wa Urusi.