1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Mpango wa Marekani wa kuweka ngao dhidi ya makombora wapinga.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6n

Rais Vladimir Putin amejibu mpango wa Marekani wa kuweka ngao dhidi ya makombora nchini Poland na jamhuri ya Cheki kwa kusitisha majukumu ya Russia chini ya mkataba wa Ulaya wa majeshi ya kawaida. Mkataba huo , uliotiwa saini mwaka 1990, unaweka kiwango cha wingi, aina na mahali ambapo hapatakuwa na silaha za kinuklia katika pande zote za eneo la zamani mataifa yaliyokuwa chini ya Urusi ya zamani.

Putin akilihutubia bunge la Russia , ameyakosoa mataifa ya magharibi wakati mawaziri wa mataifa wanachama wa NATO wanakusanyika mjini Oslo kwa mazungumzo kuhusu suala hilo la ngao, Afghanistan na Kosovo.

Walikuwa pia wanatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov.

Akizuru nchini Ujerumani jana , waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema kuwa Marekani inataka kupunguza wasi wasi wa Russia kwa kushirikiana kuhusu teknoloji ya ulinzi dhidi ya makombora. Marekani inadai kuwa ngao hiyo itakinga uwezekano wa mashambulio ya kile wanachokiita mataifa yenye ushari kama Iran.