1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Mzozo mdogo wa kidiplomasia utakwisha

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgs

Urusi imesema inawatimuwa wanadiplomasia wanne wa Uingereza wakati mzozo juu ya kugoma kwa Urusi kumrudisha mtuhumiwa wa mauaji ukizidi kupamba moto.

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema ana uhakika Urusi na Uingereza zitaondokana na kile alichokiita mzozo mdogo katika mtamshi yake ya kwanza tokea Uingereza ilipowatimuwa wanadiplomasia wanne wa Urusi mapema wiki hii.Putin amesema uhusiano madhubuti ni kwa maslahi ya nchi zote mbili lakini ni muhimu kupima hatua zao kwa kutumia busara ili kuheshimu haki za kisheria.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amevunjwa moyo na hatua hiyo ya serikali ya Urusi ambayo mbali na kuwatimuwa wanadiplomasia pia inajumuisha ufutaji wa viza kwa maafisa wa Uingereza na kusitisha ushirikiano wa kupiga vita ugaidi kati ya nchi hizo mbili.

Amesema serikali ya Urusi haionyeshi ushirikiano wowote ule mpya katika kesi ya kurudishwa kwa Bw. Andereij Lugorov kwa madai ya mauaji ya Alexander Litvinenko na anaamini kwamba uamuzi wa kuwafukuza wafanyakazi wanne wa ubalozi sio wa haki kabisa.

Uingereza iliwatimuwa wanadiplomasia wanne wa Urusi baada ya serikali ya Urusi kugoma kumrudisha Uingereza Lugovoy mtuhumiwa mkuu katika mauaji kwa kutumia miale ya sumu ya Alexander Litvinenko kachero wa zamani wa shirika la ujasusi la Urusi KGB yaliotokea mwezi wa Novemba katika mji mkuu wa Uingereza London.