1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Polisi yavunjwa maandamano dhidi ya serikali

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9m

Maandamano yaliopangwa kufanyika mjini Msocow na takriban watu 9,000 yamevunjwa na polisi kabla hata ya kuanza hapo jana.

Serikali imewatia mbaroni waandamanaji 200 ikiwa ni pamoja na bingwa wa mchezo wa dama Garry Kasparov ambaye ametozwa faini sawa na euro 30 kabla ya kuachiliwa.Wanaharakati walikuwa wamepanga kufanya maandamano dhidi ya serikali kama kilomita moja kutoka Ikulu ya Urusi kupinga kile wanachokiita ukandamizaji wa uhuru wa demokrasia unaofanywa na Rais Vladir Putin.

Hapo Ijumaa tajiri mkubwa wa Urusi anayeishi London Uingereza Boris Berezosvsky ametowa wito wa kupinduliwa kwa serikali ya Putin katika mahojiano na gazeti moja.

Hata hivyo waandamanaji wa hapo jana wamejitenganisha na tajiri huyo wa Urusi.