1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Putin aahidi kuwasaka wauaji wa mwandishi habari Anna

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4X

Rais Vladamir Putin wa Urusi ameahidi leo kwamba kila hatua inayohitajika itachukuliwa kumtafuta aliyemuua mwandishi habari wa Urusi, Anna Politkovskaya.

Anna alikuwa akiandika ripoti za uchunguzi na alikuwa mkosoaji mkubwa wa ikulu ya Kremlin.

Jamii ya kimataifa imeyalaani mauaji ya mwandishi habari huyo, na imetoa mwito uchunguzi kamili ufanywe kikamilifu na kwa haraka.

Hii leo gazeti la Novaya Gazeta limeahidi kutoa yuro laki saba na nusu kwa mtu atakayetoa habari zitakazosaidia kumkamata aliyemuua mwandishi wake.