1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Putin ataka Georgia idhibitiwe.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5D

Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa wito kwa chombo cha usalama barani Ulaya kuiwekea mbinyo Georgia kubadilisha haraka njia yake ya kushughulikia mizozo wa kimkoa.

Katika barua kwa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya , Putin amesema Georgia inataka kutatua masuala kwa nguvu.

Inafuatia kurejeshwa kwa raia wa Georgia 130 kutoka Russia, huku kukiwa na hali mbaya ya mzozo wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili.

Hali ya wasi wasi imeongezeka tangu pale Georgia ilipowakamata wanaotuhumiwa kuwa ni majasusi wanne wa Russia.

Watuhumiwa hao wote wanne waliachiliwa huru siku ya Jumatatu. Russia imeweka hatua kadha za kuiadhibu Georgia , ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahamiaji kutoka Georgia wanaoishi nchini humo kinyume na sheria.