1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Puttin asisitiza upinzani wake

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv0

Kwa mara nyingine tena rais Vladmir Puttin wa Urusi amesisitiza upinzani wake kuhusu mpango wa Marekani wa kutaka kuweka makombora ya ulinzi katika maeneo ya ulaya ya mashariki rais Puttin ameonya kuwa hatua hiyo ya Marekani itailazimisha Urusi kuweka pia makombora ya ulinzi barani ulaya.

Rais Puttin ametoa onyo hilo kabla kuanza kwa mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane tajiri zilizoendelea kiviwanda G8 unaotarajiwa kufanyika katika mji wa Heiligendamm kaskazini mwa Ujerumani.

Wote Bush na Puttin watahudhuria mkutano huo.