1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rice awasili Moscow

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0M

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Bi Condoleezza Rice amewasili mjini Moscow Urusi kuendeleza mazungumzo juu ya Korea Kaskazini. Ziara yake inafanyika kufuatia hatua ya Korea Kaskazini kutangaza kwamba mazoezi ya jeshi la Marekani kaskazini mashariki mwa Asia yanalielekeza eneo zima kuingia vitani.

Condoleezza Rice amewasili mjini Moscow akitokea Beijing China na amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov. Bi Rice anatarajiwa baadaye kukutana na rais Vladamir Putin na waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Ivanov.

Hapo awali vyombo vya habari vimeripoti kwamba utawala wa Korea Kaskazini umetangaza kwamba hautafanya majaribio mengine ya zana za kinyuklia. Hata hivyo mwanadiplomasia wa Marekani amekanusha ripoti hiyo.

Wakati huo huo, rais wa zamani wa Korea Kusini ameonya leo kwamb Korea Kaskazini huenda ichukue hatua za kijeshi kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa.