1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rice na Putin wajadili tofauti za maoni

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1k

Waziri wa nje wa Marekani,Condoleezza Rice amekutana na Rais Vladimir Putin wa Urussi mjini Moscow wakati ambapo uhusiano wa nchi hizo mbili unakabiliwa na mivutano mbali mbali.Waziri Rice hasa anataka kuondosha wasiwasi wa Urusi kuhusika na mpango wa Marekani wa kutaka kuweka makombora nchini Poland na Jamhuri ya Czech.Washington na Moscow zinatofautiana pia kuhusu mustakabali wa jimbo la Serbia la Kosovo.Lakini Putin amesema, hakuna mgongano wa maslahi na Umoja wa Ulaya. Alitamka hayo kabla ya kukutana na waziri wa nje Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya.Steinmeier amesema,pande mbili zapaswa kuondosha tofauti za maoni zilizopo,ili kuzuia mgogoro mkubwa wa kisiasa.