1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Russia na Belarusia zaafifikiana kuhusu malipo ya gesi.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeC

Russia na Belarusia zimekubaliana kuhusu malipo ya gesi saa chache kabla ya muda wa mwisho uliowekwa.

Hatua hiyo imeondoa hofu ya mataifa ya ulaya kukatiziwa huduma ya gesi.

Mkuu wa Kampuni ya Gazprom, Alexei Miller, amesema wameafikiana kuhusu malipo ya gesi na pia shughuli ya kupitishia mafuta kwenda mataifa ya Ulaya.

Waziri mkuu wa Belarusia, Sergei Sidorsky, amesema serikali yake imekubali nyongeza ya bei ya gesi ambayo imezidishwa mara mbili.

Russia imekuwa ikishinikiza nyongeza hiyo ya gesi ambapo pia ilitishia kukatiza huduma hiyo kufikia leo endapo Belarusia haingekubali nyongeza hiyo.