1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Russia yaanza tena kusambaza mafuta yake kwa nchi za ulaya magharibi.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbk

Mafuta ya Russia yameanza tena kupitishiwa nchini Belarusia kuelekea mataifa ya Ulaya Magharibi.

Hayo yamethibitishwa na serikali zote mbili.

Maafisa wa Umoja wa Ulaya walielezea kufadhaishwa na Russia pamoja na Belarusia kwa hatua ya kukatiza usambazaji wa mafuta hasa kwa kuwa Umoja huo haukutahadharishwa mapema.

Hapo awali Kamishna wa Nishati wa Umoja huo, Andris Piebalgs, aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba matatizo hayakuwa yametanzuliwa ipasavyo hata baada ya mkutano kati yao na balozi wa Russia wa Umoja huo.

Serikali ya Russia ilisitisha usambazaji wa mafuta kupitia bomba la Druzhba siku ya Jumapili kwa madai kwamba Belarusia ilikuwa ikijipatia mafuta hayo kwa njia ya udanganyifu.