1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Russia yalalamika makampuni yake kuwekewa vikwazo.

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCch

Waziri wa ulinzi wa Russia na wizara ya mambo ya kigeni wamelalamika kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya makampuni matatu ya Russia kwa madai ya kufanya biashara ya silaha na Iran

na Syria ni kinyume na sheria.

Siku ya Ijumaa, wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilichapisha orodha ya biashara 24, ikiwa ni pamoja na za Russia na nyingine nchini China, Iran na Iraq, ambazo imesema zinajihusisha na hatua ambazo zimesababisha kuwekewa vikwazo.

Vikwazo hivyo vinazihusu kampuni za Rosoboron export, ambalo ni kampuni kubwa la Russia la kuuza silaha.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Russia imepuuzia hatua hizo kuwa hazina nguvu ya kisheria. Russia na Marekani zimekuwa mara kwa mara zikigongana kuhusiana na sera za biashara na Iran katika miaka ya hivi karibuni, huku maafisa wa Marekani wakimkasirisha rais wa Russia Vladimir Putin kuhusiana na ukosoaji wa utaratibu wake wa kidemokrasi pamoja na sera za nje.