1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Russia yaweka pingamizi kwa Kosovo.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkS

Russia imeonya kuwa haitakubali pendekezo linaloungwa mkono na mataifa ya magharibi lenye lengo la kumaliza mkwamo juu ya hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo la Serbia

Juhudi za mataifa ya magharibi kumaliza mkwamo unahusu , kuipatia uhuru Kosovo iwapo muda wa mwisho wa mazungumzo ya kuleta muafaka na Serbia utamalizika.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov amesema kuwa nchi yake itaunga mkono tu azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya Kosovo iwapo Serbia pia italiidhinisha. Kosovo imekuwa ikipambana kupata uhuru kutoka Serbia , suala ambalo Serbia inalipinga moja kwa moja. Serbia iko tayari tu kuipatia Kosovo mamlaka ya ndani.