1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Uchunguzi waanza kutafuta chanzo cha ajali ya treni

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZL

Maafisa nchini Urusi wameanzisha uchunguzi kufuatia mlipuko uliosababisha treni ya abiria kuacha reli na mabehewa yake kadhaa kuanguka wakati ilipokuwa ikisafiri kutoka mji mkuu Moscow kwenda St Petersburg.

Madarzeni ya watu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo, wengine kati yao vibaya.

Akizungumza katika eneo la ajali hiyo, Sergei Wednitschenko muendeshaji mshataka wa serikali amesema, ´Ajali ya treni imesababishwa na mlipuko wa bomu lililotengenezwa nyumbani. Shirika la ujasusi FSB linachunguza kisa hicho. Tunashuku ni shambulio la kigaidi.´

Msemaji wa safari za reli nchini Urusi amesema mlipuko huo, uliotokea katika eneo la Novgord, yapata kilomita 500 kaskazini mwa Moscow, ulisabishwa na bomu.

Dereva wa treni hiyo amesema alisikia mlipuko chini ya magurudumu.