1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Ujerumani na Urusi zataka amani Mashariki ya Kati

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChS

Katika mazungumzo mjini Moscow Urusi mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani na Urusi wamekubaliana kwamba Kundi la Mataifa Manne linashoghulikia amani ya Mashariki ya Kati linapaswa kukutana hapo mwezi wa Januari.

Frank Walter Steinmeir wa Ujerumani na mwenzake Sergei Lavrov wa Urusi wameelezea wasi wasi wao juu ya hali ya mvutano ilioko kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na mapambano ya hivi karibuni kati ya makundi ya Kipalestina.Kundi hilo linazijumuisha Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya,Urusi na Marekani.

Steinmeir pia amesema anataraji kuanza mara moja kwa mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi juu ya kuanzisha upya mipango ya ushirikiano jambo ambalo lilikuwa limekwamishwa kutokana na mzozo kati ya Poland na Urusi juu ya usafirishaji nchi za nje wa nyama ya Poland.