1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Urusi yapunguza uhusiano na Hamas

1 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBdC

Serikali ya Urusi imeyakinisha uungaji mkono wa Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina kiongozi wa Fatah ambaye amekutana na Rais Vladimir Putin hapo Jumanne.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi amesema hata hivyo serikali ya Urusi itaendelea kuwa na uhusiano fulani na kundi hasimu la Kiislam la Hamas na kuendeleza mazungumzo baina ya makundi hayo katika mzozo wa Wapalestina.

Urusi huko nyuma ilikuwa na mawasiliano na makundi yote mawili ya Fatah na Hamas ambalo linahesabiwa kuwa kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya na Marekani.