1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Viongozi wa Urusi na Ufaransa kuendelea na mazungumzo leo

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H8

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amekutana na mwenyeji wake rais Vladimir Puttin wa Urusi.

Baada ya kumalizika duru ya kwanza ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika makaazi ya rais Puttin nje ya mji wa Moscow rais Sarkozy amesema kwamba wamekubaliana kuwa Iran ina uwezo mkubwa wa kutengeneza silaha za nyuklia lakini rais Puttin amesisitiza kwamba Tehran haina nia ya kutengeza silaha hiyo.

Viongozi hao watakutana leo katika ikulu ya Kremlin kuendeleza duru ya pili ya mazungumzo yao.

Marais Vladimir Puttin wa Urusi na Nicolas Sarkozy wa Ufaransa leo wanatarajiwa kujadili juu ya uhuru wa jimbo la Kosovo na swala la ugavi wa nishati kaatika nchi za Ulaya.