1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Watu 14 wauawa katika ajali ya mgodi Russia.

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByr

Watu kumi na wanne wameuawa na wengi zaidi ya hamsini wamenaswa chini ya ardhi baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe katika eneo la Kemerovo, Siberia nchini Russia.

Kiasi wachimba migodi mia moja na hamsini waliondolewa mahali hapo punde baada ya tukio hilo.

Mwezi Machi, mgodi wa karibu na mahali hapo ulilipuka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja.

Migodi ya makaa ya mawe ya Russia mara kwa mara hukumbwa na ajali ambazo zinasemekana zinatokana na mitambo ya zamani na pia upungufu wa kuwekeza kwenye sekta ya madini hayo tangu Urusi ya zamani iliposambaratika.