1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Waziri mkuu wa Israeli Ehud Olmert aiomba Rushia kuzuwia Iran isipate silaha za kinyuklia

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1O

Waziri mkuu wa Israeli Ehud Olmert, ameiomba Rushia kuzuwia Iran isipate silaha za kinyuklia. Olmert yuko mjini Moscow kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo. Kabla ya kupokewa kwa mazungumzo na rais wa Rushia,Vladimir Putin, waziri wa Rushia wa mambo ya kigeni, Sergei Lavrov, amesema kuwa anahisi hakuna haja ya kuchukua hatua juu ya mpango wa kinyuklia wa Iran. Waziri mkuu wa Israeli, Ehud Olmert, pia amesema inafaa vikwazo vya silaha viwekewe Iran na Syria ambazo zinalisaidia kundi la wapiganaji wa Hezebollah nchini Lebanon ambao walipigana vita vya mwezi na nusu na Israeli miezi mitatu iliopita.

Mnamo siku zilizopita, Rushia ilitupilia mbali pendekezo hilo la vikwazo dhidi ya Iran na Syria.