1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Yeltsin kuzikwa leo

25 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7L

Rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin kuzikwa leo hii kwa heshima zote za taifa ambapo Rais Vladimir Putin ameitangaza siku ya leo kuwa ni siku ya maombolezo ya taifa.

Waombolezaji wamekuwa wakitowa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Yeltsin ambao umelazwa kwenye kanisa la Yesu Muokozi katikati ya jiji la Moscow.Yeltsin alikuwa rais wa kwanza wa Urusi alieachaguliwa kidemokrasia hapo mwaka 1991 na alitumikia wadhifa huo hadi pale alipojiuzulu mwaka 1999 na kuacha nyuma urithi tafauti.

Wakati ameiweka Urusi kwenye njia ya demokrasia na uchumi unaotegemea nguvu za soko pia ameanzisha vita vya kwanza dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga huko Chechnya ambavyo vimemalizika kwa Urusi kuyaondowa majeshi yake kwenye jimbo hilo.

Yeltsin alifariki dunia hapo Jumatatu akiwa na umri wa miaka 76.

Ujerumani itawakilishwa katika maziko hayo na Rais Horst Köhler.